Categories: ABC Articles

LESENI NA VIBALI VYA FILAMU TANZANIA

LESENI NA VIBALI VYA FILAMU TANZANIA

Kwa mujibu wa Sheria Na. 4 ya mwaka 1976 ya Filamu na Michezo ya Kuigiza, filamu zote za ndani na nje ya nchi zinapaswa kukaguliwa na kupewa vibali na leseni ya kuonyeshwa nchini, pia filamu hizo zitapewa madaraja kwa kuzingatia tamaduni, mila na maadili ya Kitanzania.  Wazalishaji wote wa filamu nchini watatakiwa kupeleka nakala ya filamu zao kwa ajili ya                                                                                                                                                                                                                                                                                                        ukaguzi kisha kupata/kutopata kibali kutoka kwa bodi ya filamu hili kuweza kuzalisha na kusambaza filamu zao. Maombi ya kibali au leseni ya kufanya shughuli zinazohusiana na filamu na michezo ya kuigiza nchini kwa wazalishaji Wazawa yataambana na;

  • Barua ya maombi ya kutengeneza filamu;
  • Fomu za maombi ya leseni/kibali pamoja na taarifa za wasanii watakaocheza filamu husika, gharama, na idadi ya nakala zitakazozalishwa;
  • Miswada na kazi zilizokwishazalishwa kwa ukaguzi mfano: VHC, DVD, CD nk;
  • Ada ya kibali ambayo ni 1,000,000/= (Shillingi Milioni moja) kwa huduma ya haraka na 500,000/= (Shillingi Milioni Moja) huduma ya kawaida.

Maombi ya kibali/leseni ya kufanya shughuli zinazohusiana na filamu na michezo ya kuigiza kwa wazalishaji kutoka nje ya Tanzania yataambana na;

  • Fomu ya maombi ya uzalishaji filamu ambayo lazima isainiwe na Ubalozi wa Tanzania katika inchi anayotoka pamoja na taarifa za timu yake yote ya uzalishaji filamu;
  • Picha aina ya passport size;
  • Kivuli cha hati ya kusafiria ya muombaji;
  • Nakala ya muswada wa filamu inayotarajiwa kutengenezwa;
  • Ada ya kibali ambayo ni $3000 kwa huduma ya haraka na $1000 huduma ya kawaida.

Filamu zote zitakazozalishwa ndani ya nchi zitakaguliwa na kupewa kibali kabla ya kuonyeshwa sehemu yoyote nchini, ukaguzi huu utakagharimu Tshs 1,000 kwa dakika kwa filamu itakayozalishwa na mzawa na $5 kwa dakika kwa filamu iliyozalishwa na mtayarishaji asiye mzawa. Mara baada ya ukaguzi huu filamu itapewa daraja, kama inavyoonekana kwenye jedwali hapa chini;

Daraja Maelezo
U Filamu katika daraja hili inafaa kutazamwa na watu wa rika zote
A13 Filamu katika daraja hili inafaa kutazamwa na watoto walio na umri wa miaka 13 wanapokuwa na watu wazima

 

A16 Filamu katika daraja hili inafaa kutazamwa na watoto walio na umri wa miaka 16 wanapokuwa na watu wazima

 

A18 Filamu katika daraja hili inafaa kutazamwa na watu walio na umri wa miaka 18
R Imekataliwa (rejected)
X Filamu hizi haziruhusiwa kabisa nchini Tanzania

 

Pia, bodi ya filamu itatoa leseni ya kuonyesha filamu katika Kumbi/ Majumba ya Sinema. Maombi ya leseni ya kuonyesha filamu katika sinema nchini yataambana na; Barua ya maombi ya kibali cha uendeshaji wa kumbi/jumba la sinema kwa Bodi kuu na bodi za wilaya zitakazokagua ukumbi/jumba lililoombewa kibali kama linakidhi viwango vya kiafya, kiusalama na kimiundombinu kwa mujibu wa taratibu na kanuni.Bodi ikiridhika kua muombaji amekidhi vigezo stahiki itatoa daraja kwa ukumbi.

admin

Recent Posts

New Regulations on Business Licensing: Key Updates for Entrepreneurs

New Regulations on Business Licensing: Key Updates for Entrepreneurs Introduction: In a significant development for…

1 year ago

Legal Update: Key Points on the Foreign Exchange (Amendment) Regulations, 2023

Legal Update: Key Points on the Foreign Exchange (Amendment) Regulations, 2023 Key Points: - The…

1 year ago

Legal Update: New Regulations on Companies’ Beneficial Ownership

Legal Update: New Regulations on Companies' Beneficial Ownership Key Points: 1. The Companies (Beneficial Ownership)…

1 year ago

The Personal Data Protection (Personal Data Collection and Processing) Regulations, 2023

The Personal Data Protection (Personal Data Collection and Processing) Regulations, 2023 By Sunday Ndamugoba and…

1 year ago

The Personal Data Protection (Complaints Settlement Procedures) Regulations, 2023.

The Personal Data Protection (Complaints Settlement Procedures) Regulations, 2023. By Sunday Ndamugoba and Lubaina Hassanali…

1 year ago

Overview of The Personal Data Protection Act 2022 of Tanzania

Overview of The Personal Data Protection Act 2022 of Tanzania By Sunday Ndamugoba and Lubaina…

1 year ago