- December 29, 2020
- Posted by: admin
- Category: ABC Articles
USITISHWAJI WA AJIRA TANZANIA.
MASWALI
- Nini maana ya usitishwaji wa Ajira?
JIBU
Usitishaji wa ajira una maana ya ukomo wa mkataba au mahusiano ya kiajira baina ya mwajiri na mfanyakazi/Mwajiriwa.
- Kuna aina ngapi za usitishwaji wa ajira?
JIBU
Kuna aina Mbili za usitishwaji wa ajira ambazo ni,
(i) Usitishwaji wa ajira kwa Haki
(ii) Usitishwaji wa ajira pasipokuwa na haki?
- Je ni sababu zipi zinapelekea Mfanyakazi kusitishiwa ajira yake Kwa Haki?
JIBU
(a)Kutoa Siri za Ofisi yake afanyiayo Kazi na Shughuli Zake.
(b)Kuthibitika amefanya Wizi kwenye mali ya mwajiri wake. Hivyo kukutwa na kosa la jinai, pia lazima ithibitishwe akiwa ametenda kosa hilo.
(c) Utovu wa nidhamu mahali/sehemu ya kazi.
(d) Utoro kazini kwa zaidi ya siku tatu.
(e) Kushindwa kutunza kumbukumbu za ofisi.
- Je ni sababu zipi zinapelekea Mwajiriwa kusitishiwa ajira yake bila Haki?
JIBU
(a) kuondolewa/kusitishwa kwenye ajira bila kupewa onyo kulingana na kosa alilotenda muajiriwa.
(b) Kusitishwa kwenye ajira bila kupewa sababu za msingi za usitishwaji wa ajira.
(c) Kusitishwa kwenye ajira bila kupewa nafasi ya kujitetea kulingana na kosa alilolifanya mfanyakazi/mwajiriwa.
- Ni stahiki zipi mwajiriwa anazipata baada ya kusitishiwa ajira yake bila haki au kufatwa utaratibu?
JIBU
Stahiki ambazo anastahili kuzipata mwajiriwa baada ya kusitishiwa ajira yake pasipo haki ni Kama zifuatazo:
(a) Kulipwa fidia ya mishahara yake isiyopungua miezi kumi na mbili (12)
(b) Kurejeshwa kwenye ajira na kulipwa mishahara bila kuwapo na hasara Kwa kipindi ambacho mwajiriwa hakuwepo kazini kutokana na kusitishwa kwa ajira bila kufata haki.